Mwanamke mwenye Ulemavu, Bi. Mwashi Bedo, akipanga vyombo na vitu vyake vilivyochukuliwa
kwa mabavu na viongozi wa Kijiji cha Serengeti-Wilaya ya Bunda, lakini baadae wasaidizi
wa Kisheria walimsaidia kupata haki yake na kumrudishia vyombo vyake.
Na MwandishiWetu, Bunda
Bi. MwashiBedo (50) ni mwanamke
mwenye ulemavu wa miguu na viungo, anaishi katika kijiji cha Serengeti,
WilayayaBunda. Kama ilivyo kwa watu wengi wenye ulemavu nchini Tanzania, Bi.
Mwashi anaishi katika mazingira magumu kwa sababu ya kukosa kipato cha kutosha kumuwezesha
kujitunza yeye mwenyewe binafsi na kutunza familia zao. Lakini, Bi. Mwashi amepata
bahati ya kuzaa mtoto wa kiume, Michael Mathayo (14), ambae anamtunza mama yake
na familia yao kupitia biashara ndogondogo na kazi za vibarua katika mashamba ya
watu anazofanya hapo vijijini.
Kama njia ya kuharakisha utekelezaji
wa maendeleo ya miradi mbalimbali kijijjini, uongozi wa Kijiji cha Serengeti
umetengeneza kanuni na taratibu ambazo zinamtaka/zinamlazimu kila mwanajiji kuchangia
aidha fedha au nguvu kazi, katika mradi wowote wa maendeleo wa kijiji unaobuniwa.
Miakamiwiliiliyopita,
uongozi wa kijiji ulibuni mradi wa kujenga shule ya sekondari, na kumtaka kila mwanajiji
kuchangia shilingi elfu 10 ili kufanikisha ujenzi huo. Kijiji kilihamasishwa kuchangia
fedha au nguvu, kwa kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji.
Wana kijiji wengi walihamasika
kuchangia fedha za ujenzi wa shule hiyo, lakini Bi.Mwashi alishindwa kuchangia fedha
au nguvu kwa ajili ya mradi huo, kutokana na umaskini na hali ya ulemavu aliyonayo.
Bila kujali ulemavu wake na hali
ya maisha iliyonayo, viongozi wa Kijiji cha Serengeti walikwenda nyumbani kwa
Bi. Mwashi, na kuchukua (kwa nguvu) vyombo na vitu vyake vya ndani—meza, viti,
na vinginevyo, lengo kuu likiwa ni kuuza vyombo hivyo ili kufidia fedha (10,
000/=) aliyopaswa kuchangia Bi.Mwashi katika mradi wa shule ya sekondari ya kijiji.
Bi.Mwashi alijitaidi sana kuwasihi
viongozi wa kijiji kumrudishia vyombo vyake, lakini juhudi zake hazikuweza kuzaa
matunda kwa sababu viongozi hao bado waliendelea kushikilia vyombo hivyo na kuendelea
na mpango wao wa kuviuza ili kufidia fedha alizopaswa kulipa Mlemavu huyo kama mchango
wa ujenzi wa shule.
Baada ya kukasirishwa na maamuzi
yaliyofanywa na viongozi wa kijiji, baadhi ya wawanakijiji waliungana na kwenda
kumshauri Bi. Mwashi kupeleka malalamiko yake kwa Msaidizi wa Msaada wa Kisheria—Bunda,
ili aweze kusaidiwa. Msaidizi wa kisheria alimpeleka Bi.Mwashi kwenye Ofisi za Ustawi
Jamii na MkuuwaWilaya wa Bunda, ambazo ziliandika barua rasmi iliyowaelekeza uongozi
wa Kijiji cha Serengeti kurumrudishia Bi. Mwashi vyombo vyake vyote na kumuondoa
kabisa kwenye orodha ya wanakijiji wanaopaswa kuchangia fedha au nguvu katika mradi
wowote wa kijiji wa sasa na ijayo.
Viongozi wa Kijiji walitii agizo
la Mkuu wa Wilayana Afisa Ustawi wa Jamii, na baadae walirudisha vyombo vyote walivyochukua
katika nyumba ya Bi. Mwashi, na kuondoa jina lake katika orodha ya watu wanaopaswa
kuchangia katika miradi mbalimbali ya kijiji.
“ Nawashukurusanawasaidiziwakish eria,
wamepiganampakavyombonavituvya nguvimerudi. Jambo hili limenipafaraja ya moyo…na
sasa hivi hakuna kiongozi yoyote wa kijiji anayekuja nyumbani kwangu kudai mchango
wowote wa mradi wa kijiji,” amesemaMwashi.
Baada ya kurudishiwa vitu
vyake na kupata hakiyake, Mlemavu huyu anaendelea na maisha yake ya kawaida
(kwa msaada wa mwanae Michael), ambae anafanya kazi za vibarua katika mashamba ya
watu na kufanya shughuli ndogondogo—zinazowawezesha kupata kipato cha kujikumu na
kupata mahitaji mbalimbaliyamsingi.
Akiongelea jinsi Mwanamke Mlemavu
huyu alivyoteseka na hatimae kupata haki yake, Mtaalam wa Maswala ya Ustawi wa Jamii,
Bi. Anna Kitojo, amesema “Watu wenye ulemavu na familia zao wanakabiliwa na changamoto
lukuki. Wasaidizi wa kisheria na wadau wengine wa msaada wakisheria na maendeleo
wanapaswa kuunganisha nguvu ili kuwakwamuwa kutoka katika matatizo haya,
kuboresha maisha yao,na kuwawezesha jamii
ya watu wenye ulemavu kutimiza ndoto zao za maisha.”
No comments:
Post a Comment