Waziri wa Maji, Pro, Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha inamaliza kero ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ifikapo mwaka 2020 iwe imefikisha asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 vijijini, wananchi wapate huduma ya maji safi na salama.
Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kufunga wiki ya maji na kufungua kikao cha tathmini ya wataalamu wa maji, wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na wafadhili waliokutana Jijini Dodoma kuangalia namna ya kukabiliana ya changamoto ya utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
Waziri Mbarawa amesema serikali imeweka msukumo mkubwa kuhakikisha wanatatua kero za ukosefu wa maji safi na salama kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maji mijini na vijijini.
“Serikali imejipanga kuhakikisha kero ya maji inapungua kwa kiasi kikubwa kama utaona tunatekeleza miradi mikubwa ili kuhakikisha tunatatua changamoto hii, ikiangalia serikali inatekeleza takribani miradi 500 kwa nchi nzima, ambayo itapeleka maji safi na salama mijini na vijijini”
“Tuna mradi mkubwa unaogharimu kiasi cha zaidi ya bilioni mia sita ambao utapeleka maji maeneo ya Tabora, Shinyanga, Nzega na Igunga ambao utatoa maji Victoria na kupeleka maeneo hayo, pia amesema kuna zaidi ya bilioni mia tano ishirini na tano ambao utapeleka maji safi na salama Jijini Arusha kwahiyo kwa kiasi kikubwa serikali imewekeza nguvu nyingi sana kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salam” amesema Pro, Mbarawa.
Aidha Profesa Mbarawa amebainisha kuwa adhima ya serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020, kwa maeneo ya mijini wapate maji kwa asilimia 95 na upande wa vijijini wapate kwa asilimia 85.
Na amebainisha kuwa mpaka sasa kwa upande wa vijijini ni asilimia 64 ndio wanaopata maji safi na salama, huku wa maeneo ya mijini angalau kuna baadhi ya miji imevuka lengo, waziri Mbarawa pia amesema awali kulikuwa na changamoto ya utoaji huduma hiyo lakini kwa sasa wametunga sheria mpya ambayo italahisisha kufikia malengo kwa haraka.
“Ukiangalia hapo mwanzo tulikuwa na changamoto kwenye kukabiliana na tatizo hili lakini kwa tumetunga sheria mpya ambayo itasimamia upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa maeneo ya mijini na vijijini lengo la serikali kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi na salama” amesema Mbarawa.
Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi kutoka wizara ya maji Silvesta Matemu, amesema wao kama wataalamu wanawajibu wa kutekeleza mipango ya sera ya maji, na kuwaomba wananchi kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji.
Amesema waziri ana toa sera na wao kama wataalamu wanakuwa na wajibu wa kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa vizuri na huduma ya maji safi na salama inapatikana kwa wananchi.
Pia amewaomba wananchi kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji ili hata mamlaka husika yenye wajibu wa kulinda vyanzo hivyo kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa jamii, amesema ulinzi wa vyanzo vya maji ni wajibu wa kila mtu.
Nae Mkurugenzi wa kitengo cha uratibu program sekta ya maji Donsia Mwashamu amesema wiki ya maji imeadhimishwa kwa vipengere vitatu ambapo kwanza ilikuwa tarehe 18 kulikuwa na kongamano la kisayansi, na 20-21 Ewura walikuwa wanatoa taarifa ya maji na utekelezaji wake.
Na leo ilikuwa ni kilele na kutathmini kwa yale ambayo yamejadiliwa katika wiki nzima na kujithmini katika hali ya utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi wapi tulipotoka na wapi tunaelekea kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi mijini na vijijini.
No comments:
Post a Comment