BENKI ya NBC imesema itaendelea kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi ili kuweza kukidhi mahitaji ya wale wanaohitahi huduma za kibenki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Shika Ndinga, Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC, Benjamin Nkaka alisema lengo la NBC ni kutaka kila mwananchi afikiwe na huduma za kibenki kwa urahisi na ukaribu.
Alisema moja ya huduma inayopatikana katika kampeni hiyo ni ufunguaji wa akaunti yao mpya ya Fasta inayomwezesha mteja kupata kadi ya ATM aina ya Visa muda huo huo naofungua akaunti.
Alisema akaunti ya Fasta inafunguliwa na kiwango cha chini cha shs 5000/- na hata kama mtu hana kiasi hicho anaweza kufungua bila pesa yoyote na kasha akaweka pesa siku inayofuata hata kwa kutumia simu yake ya mkononi
"Hii ni hatua nyingine katika maendeleo ya teknolojia za kibenki hapa nchini mteja kufungua akaunti na kupewa kadi ya ATM Visa hapo hapo, NBC itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kubuni na kuingiza sokoni bidhaa zinazokwenda na wakati na kukidhi mahitaji ya wateja wetu,” aliongeza Bwana Nkaka.
Pamoja na akaunti ya Fasta, Mkuu huyo akiongeza kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata suluhisho katika mahitaji yao ya maisha ya kiula siku NBC inaendelea kufanya vizuri na kuhimiza watanzania kujiunga na akaunti ya Malengo ya benki hiyo.
“Tunatambua kila binadamu anngependa kutimiza malengo ya maisha na ndoto yake, akaunti ya Malengo ya NBC ni suluhisho litakalomwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo itakayomsaidia kutimiza mahitaji yake iwe ni ada za shule, kodi za nyumba na mahitaji mengine,” aliongeza Nkaka.
“Natoa wito kwa watanzania kuja kufungua akaunti la Malengo ili kutimiza malengo ya ndoto zao na pia tumewaletea akaunti ya Fasta hivyo kufungua akaunti ya benki hakuhitaji tena foleni na vigezo lukuki bali ni kitambulisho chako tu cha NIDA, Kura ama leseni ya Udereva,” akaongeza.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Saĺaam aliyefungua akaunti ya Fasta, Jumanne Abdallah aliipongeza NBC kwa huduma hiyo kwani ameweza kupata akaunti na kadi ya ATM ya Visa ndani ya dakika tano.
No comments:
Post a Comment