Machi 19, 2019 - DTB-Tanzania imeweka historia kwa kuzindua huduma 3 ambazo zitaongeza ufanisi katika jitihada za kuwafikia wateja waliombali na matawi na kupunguza gharama za kupata huduma za kibenki kwa wateja wake. Huduma zilizozinduliwa hivi karibuni ni pamoja na Prepaid Card, DTB wakala na Merchant Payment devices (POS).
Kadi hizi za Pre-Paid ambazo zipo kwenye mfumo wa MasterCard, zina uwezo wa kubeba fedha aina kumi zinazotambulika kimataifa tofauti na Shilingi ya Tanzania ambayo ni fedha namba moja. Hivyo kadi hizi zinafaa kwa wafanyabiashara wanaosafiri nje ya nchi kwa matibabu, wanafunzi wanaosoma nje ya nchi na watalii. Fedha hizi ni pamoja na Dola za kimarekani, Yuro ya bara la Ulaya, Paundi ya Uingerereza, Dirham ya Ufalme za Kiarabu, Rupee ya India, Randi ya Afrika Kusini, Yuan ya Uchina, Dola ya Canada na Shilingi za Kenya na Uganda.
Kadi hizi za Pre-Paid zipo kwenye teknolojia ya hali ya juu ili kuimarisha usalama kwa wateja na haziwezi kughushiwa kwa namna yoyote.
No comments:
Post a Comment