Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amemuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki kwa kushindwa kudhibiti matukio ya uhalifu likiwamo wimbi la mauaji ya watoto, mkoani humo hivi karibuni.
Uamuzi huo aliutangaza juzi jioni alipozungumza na wananchi mjini Lamadi Wilaya ya Busega ambapo amesema amechukua uamuzi huo baada ya kamanda huyo kulalamikiwa na wananchi kushindwa kudhibiti hali hiyo.
“Kutokana na matukio hayo tayari nimemwondoa aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa, Deusdedit Nsimeki na kumleta mwingine (hakumtaja jina),” alisema IGP Sirro.
Hadi sasa imeripotiwa watoto watatu na wanawake wawili wameuawa na kunyofolewa baadhi ya viungo vyao tangu Oktoba 10 mwaka jana hadi mwaka huu. Matukio hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na mpaka sasa watu 12 wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuhusika katika matukio hayo.
No comments:
Post a Comment