Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. Watatu (wapilikulia) Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani ambae amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Wengine ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Jehud Ngolo pamoja na Sophet Mafuru kutoka SMSRTCODES LTD hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Benki ya CBA na Vodacom kwa mara nyingine wamewaletea Watanzania na wateja wake promosheni kubwa ya mwaka inayojulikana kama Shinda na M-PAWA. Promosheni hii itaibua washindi 200 kila wiki watakao ongezewa mara mbili ya akiba zao pia kutakuwa na washindi 15 watakaoweza kurudisha mkopo kabla ya siku thelathini kujinyakulia shilingi 100,000/= kila wiki. Zawadi kubwa zitakazotolewa kwenye droo kubwa wiki ya sita zitakua ni kitita cha Milioni 10 taslimu na Bajaj tano.
Zaidi ya washindi 1300 watajinyakulia zawadi mbali mbali (za kifedha na Bajaji) ambazo zote kwa ujumla zitakuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100.
Promosheni hii inaonyesha jitihada za CBA Bank na Vodacom kuleta muamko wa kifedha na kuhimiza Watanzania kuwa na tabia ya kuweka akiba. Akizungumza wakati wa uzinduzi kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CBA Julius Konyani alisema “M-PAWA ni bidhaa inayoendelea kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa Watanzania hasa wale wamiliki wa biashara ndogo wanaoweka akiba na na kupata riba na Pia kupata mikopo inayowasaidia katika kuendeleza na kukuza biashara zao”.
Promosheni hii ya Shinda na M-PAWA itaendeshwa kwa muda wa wiki sita kuanzia Novemba 2018 hadi nusu ya Desemba 2018.
Meneja Masoko wa Vodacom Huduma za kifedha Noel Mazoya alisema “Wateja watakaoomba mkopo na kurudisha mapema watakuwa na nafasi ya kuopoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa wateja 15 kila wiki na Jumla ya wateja 96 watashinda kwa wiki sita. Tunajenga utamaduni wa kuhimiza Watanzania kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukuza biashara zao. Hata hivyo hatuwahimizi tu wateja wakope, lakini pia kurudisha mikopo mapema. Hii itawapa wateja fursa ya kuomba tena mkopo na kuongeza kiwango wanachoweza kukopa” alisema haya wakati wa tukio la droo ya kwanza lililoshuhudiwa na Bodi ya bahati nasibu Tanzania pamoja na watendaji wengine wa CBA.
Mpawa ni Huduma inayotolewa kwa ushirikiano wa Bank ya CBA na Vodacom, Huduma hii inawewezesha wateja kuweka fedha kwenye Mpawa na Kupata Riba/faida. CBA imekuwa mmojawapo ya benki inayowekeza nchini ambapo kuptia huduma hii imefanikiwa kuwafikia wateja zaidi ya milioni saba, wakiwa ni wateja wadogowadogo ambao wanahifadhi kiwango cha kati ya shilingi 1000/= na 3000/=. Viwango ambavyo mfumo wa kibenki wa kisasa usingeweza kuwahudumia, Huduma hii ya mpawa imeifikia jamii kubwa ambayo haipo kwenye mfumo rasmi wa kifedha (Financial Inclusions). CBA Bank na Vodacom zitaendelea kuwekeza nchini na wanatoa wito kwa wateja wote wa Vodacom/Mpesa kuweka hela zao katika kibubu chao cha mpawa ambacho ni salama na benki yao mkononi mwao, Pia wanaweza kukopa kiwango chochote kati ya shilingi 1000 mpaka laki tano.
No comments:
Post a Comment