A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 7, 2018

Wananchi waliojenga ndani ya hifadhi za mipaka ya kimataifa kuondolewa

Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro


Erikali imewaagiza wananchi waliojenga na kuishi ndani ya hifadhi ya mipaka ya kimataifa kati ya kenya na nchi nyingine jirani kuondoka mara moja kwa hiari kwa kuwa wamevamia mipaka hiyo.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi mheshimiwa william lukuvi katika ziara yake ya siku moja ya kukagua mpaka kati ya tanzania na kenya katika maeneo ya tarakea, rongai na holili wilaya ya rombo mkoani kilimanjaro.

Mh lukuvi amesema, hatua hiyo pia itawahusu wananchi wa nchi jirani ya kenya na nchi nyingine zinazopakana na tanzania na kwamba serikali hivi sasa imo katika mchakato wa kuhakiki na kuweka mipaka yake upya katika nchi hizo.

Katika taarifa yake mkuu wa wilaya ya rombo bi agness hokororo amesema, wananchi hao walielimishwa lakini walikaidi na kuwasilisha malalamiko yao kwa waziri mkuu baada ya nyumba zao kuwekewa alama za x za kutakiwa kuvunja nyumba zao.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambayo wamesema itasaidia kupunguza vitendo vya biashara ya magendo, wizi ukiwemo wa mifugo na kuvushwa nchi jirani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages