A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 8, 2018

Trump atoa maneno makali kuelekea mkutano wa G7


Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada na, kwamba inatoza ushuru mkubwa kwa bidha zitakazo Marekani na kusabisha mazingira magumu yasiyoenda na sera za kifedha.

Kitendo cha Trump kuongeza tozo katika bidhaa za chuma kumemuweka katika mazingira ya kutofautiana na mataifa wanacha wa G7.Akizungumza awali na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau mjini Ottawa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwaambia waandishi wa habari kwamba watatumia mkutano ujao wa G7 kumshawishi rais Trump dhidi ya msimamo wake kibiashara.

Nitarudia kumwambia rais Trump kwamba hatua alizochukua hazina manufa hata kwa uchumi wa taifa lake.Kwa mimi hili ni jambo lililowazi,huwezi kuanzisha vita vya kibiashara na washirka wako.Sisi sote tunashirikiana katika mzozo wa Syria na Iraq na maeneo mengine duniani.Ni washirika na tunabadilishana taarifa,majeshi yetu yanashirikiana kulinda uhuru wetu.Katika mazingira ya kimataifa tunayokabiliana kwa siku za leo hatuwezi kuanzisha vita vya kibiashara miongoni mwetu.Nitajaribu kumshawishi kurejea katika hali ya kawaida kibishara na kuondoa hali hii ya hofu kibiashara."Anasema Macron.

Hata hivyo Macron amesisitiza kuwa bado muungano wao unaweza kusonga mbele hata bila Marekani kama italazimika kuwa hivyo.

" Labda Rais Trump hajali kuhusiana na kujitenga kwake,lakini hatujali tupo tayari hata kuwa mataifa sita,kama itabidi kwa sababu mataifa hayo sita yanawakilisha umoja wetu na hadhi yetu yenye manufaa kwa mjibu wa historia ya muungano huu na dunia ya sasa."ameongeza Macron

Hatua ya hivi karibuni ya Rais Trump ya kuongeza tozo kwa bidhaa kwa washirika wake kumezua mzozo mpya wa kibiashara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages