A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 5, 2018

KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YAJINYAKULIA TUZO


Jumla ya Tuzo tano walizopata Green West Pro ndani ya miaka mitano mfululizo kwa kushika nafasi ya Kwanza.
Na Anna Chiganga Utouh news.
Kampuni ya usafi na utunzaji mazingira nchi Tanzania Green West pro katika kuazimisha siku ya mazingira Dunani umeitaka jamii kutambua thamani ya taka na  kuhifadhi mazingira kwa kujipatia kipato kutokana na aina mbalimbali za taka.

Hayo yamesemwa na Meneja uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Abdalah Mbenna alipokuwa katika uwanja  wa mnazi mmoja katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambapo kitaifa yame fanyika  jijini Dar es Salaam na kuitaka jamii kufahamu umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi.

Amesema kampuni hiyo imepata ushindi katika makampuni ya usafi na mazingira Tanzania na kujinyakulia tuzo tano kwa muda wa miaka mitano, ambapo mwaka huu pia imepata tuzo na cheti cha mshindi wa kwanza.

Kampuni ya Green Waste Pro inatoa Huduma zake katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages