A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 4, 2018

MURKAZ TABLIGH YATOA MSAADA WA FUTARI CHALINZE


 MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete,  amepokea msaada wa futari kutoka kwa taasisi mbili za kidini ya kiislam, kwa ajili ya Waislamu waliopo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani jimboni humo.


Akipokea msaada wa futari hiyo iliyotolewa na taasisi za Dar Irushad Islamia Markaz na Miraj Islamic Centre za jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wananchi wasiojiweza, mbunge huyo amesema msaada huo utawafikia walengwa na kuzishukuru taasisi hizo kwa kuwakumbuka wananchi wanaoishi katika mazingira magumu katika mwezi wa Ramadhan.

Kwa upande, Arif Yusuf wa taasisi moja miongoni mwa zilizokabidhi misaada hiyo, ameeleza kwamba mwezi huu wa Ramadhan ni wa kumtegemea Mwenyezi Mungu na hivyo wameona ni vyema kula futari na wananchi wasiojiweza wa jimbo la Chalinze lakini akasema kwamba na wao misaada hiyo huipokea kutoka kwa taasisi mbalimbali za nje  ikielekezwa kuwaendea wasiojiweza.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages