NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA amewataka watendaji wa Manispaa hiyo na Watumishi wake kufanya kazi kuacha kubweteka.
Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao maalum kilichoandaliwa na manispaa ya Ilala cha kutoa majibu ya ufafanuzi wa kero zilizowasilishwa wakati wa ziara ya MWENYEKITI WA Chama cha mapinduzi mkoa wa Dar esSalaam Cathe Kamba.
"Nawakumbusha kila mtumishi kusimamia majukumu yake msivuke mipaka katika utekelezaji wa kazi zenu. "alisema Mjema.
Alisema watumishi na Watendaji wa Ilala watakaokiuka misingi ya kazi watachukuliwa hatua Kali.
Amewataka wafanye kazi kwa weledi pia washirikiane katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Ilala.
Alisema kikao hicho kilikuwa kinawahusisha watendaji wa idara zote za I LALA wakiwemo chama na serikali, Idara, AFYA, Mazingira, Maendeleo ya Jamii, Tasaf, elimu msingi na sekondari ,idara ya usafishaji, ambapo zote zilitolewa majibu.
Kwa upande wake Katibu wa ELIMU na mazingira jumuiya ya Wazazi WILAYA ILALA Wilson Tobola alipongeza ofisi ya mkuu wa WILAYA ILALA
Kutolewa majibu ya kero zilizojitokeza katika ziara ya MWENYEKITI wa CCM Mkoa.
Tobola Alisema tumepokea kwa Furaha majibu hayo wanasubiri utekelezaji wake watendaji wa serikali tunawaomba wawajibike wasikae ofisini washuke chini kusikiliza kero za wananchi.
"Tunawaomba watumishi wetu wa Ilala washirikiane na mkuu wetu wa WILAYA
Kutatua changamoto pia waweke utaratibu wa kutembelea wananchi kila mwenye idara yake "alisema Tobola.
Alisema kwa upande wa chama na jumuiya ya Wazazi wameaidi kupokea maelekezo na kuyafanyia kazi kwa ushirikiano wa ofisi ya wilaya ILALA kwa faida ya wananchi.
Alimpongeza mkuu wa wilaya Ilala SOPHIA MJEMA kwa kuwaunganisha jumuiya zote pamoja na chama cha mapinduzi CCM.
No comments:
Post a Comment