
Kikosi cha Yanga.
HATIMAYE Yanga jana ilifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza baada ya kupita mechi tisa za kimashindano tangu aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina, aachane nao.
Jana Jumanne, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Bao hilo lilifungwa dakika ya 26 na kiungo wake, Thabani Kamusoko kwa njia ya faulo.

Kikosi cha Mbao
Kabla ya mcheÂzo huo wa jana, Yanga ilikuwa imecheza mechi tisa za kimashindano bila ya ushindi zaidi ya kuaÂmbulia sare na kufungwa. Mechi hizo ni za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa ushindi huo, Yanga wameÂfikisha pointi 51 wakiwa katika nafasi yake ya tatu, huku Simba wakionÂgoza wakiwa na pointi 68. Azam FC ni ya pili ikiwa na pointi 55.
No comments:
Post a Comment