Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha amemkingia kifua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hakuwahi kukataza waanafunzi waliopata mimba kuzuiwa kuendelea na masomo na badala yake ni kusisitiza kilichoamuliwa tangu 2002.
Ole Nasha amelazimika kufanya jambo hilo leo bungeni wakati alipokuwa akimjibu mbunge wa Suzan Lymo ambaye alikuwa akitaka majibu ya namna serikali ilivyojipanga kuhusu zile sababu zilizo nje ya uwezo wa wanafunzi kuhimili kubeba mimba zinapatiwa ufumbuzi ikiwa tayari kuna tamko la kuzuia wanafunzi wasiendelee na shule lililotolewa na Rais Magufuli 2017.
Akijibu swali hilo Mh. Ole Nasha amesema kwamba Serikali imefanya marekebisho ya sheria ya elimu sura 363 ambapo imeongeza kipengele cha mtu yoyote ambaye atamuweka ujauzito mwanafunzi atafungwa miaka 30.
Mh. Nasha amesisitiza kuwa "Naomba nimsahihishe Mh. Lymo kwamba katazo lilikuwepo tangu 2012. Rais hajakataza wanafunzi waliopata ujauzito kutokuendelea na masomo. Alichokifanya ni kusisitiza kitu ambacho kilishaamuliwa siku nyingi." - Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha.
Aidha ameongeza kwamba "Serikali imeamua kuchukua uamuzi wa kuwazuia wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo, kwa lengo la kuwalinda, kwani wanaporejea shuleni hunyanyapaliwa na wenzao jambo ambalo huwaathiri kisaikolojia".
"Tunataka kuweka wazi kwamba, hatutegemei wanafunzi wetu katika umri mdogo waendelee kufanya mapenzi wakiwa mashuleni, kwa sababu inawaathiri katika masomo yao. Tumeamua kuchagua hatutaki kuchanganya mapenzi na elimu katika umri huo mdogo." ameongeza
No comments:
Post a Comment