Bi. Theresia akitoka kukagua Jengo la Ujenzi wa Madarasa 4, ya Gorofa katika Shule ya Gerezani.
Katibu Tawala Mkoa akiweka Saini katika kitabu cha Wageni katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo Manispaa ya Ilala .
Katibu tawala Mkoa akikagua baadhi ya Madarasa yaliyokarabatiwa katika shule ya Uhuru mchanganyiko iliyopo Manispaa ya Ilala ambapo Ukarabati wa Vyumba 27, vya Madarasa kumbi 2,Pamoja na Jengo la Utawala katika shule hiyo,
Ujenzi ukiendelea Katika Shule ya Sekondari Gerezani ambapo ni Ujenzi wa madarasa manner ya Gorafa.
Baadhi ya vyoo katika Shule ya Sekondari Gerezeni.
Ujenzi wa madara 4 ya gorofa Shule ya sekondari Gerezani ambapo ujenzi huo unaendelea.
Rs Bi. Theresia Mmbando akikagua vyoo katika shule ya Msingi Ilala.
Mradi wa ukarabati wa Matundu ya Choo katika shule ya Msingi Ilala ambapo kwa sasa unakaribia kukamilika,ambapo mradi huo ulianza March 13, mwaka huu.
Picha ya Pamoja wajumbe kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipofanya Ziara katika shule ya msingi Ilala ambapo imeongozwa na Katibu Tawala Mkoa (RS) wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Na Anna Chiganga Utouh news.
Katibu Tawala Mkoa Bi. Theresia Mmbando akishirikiana na wakuu wa Idara pamoja na Watumishi kutoka katika Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam, leo wamefanya Ziara kukagua Miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo wameangali Utekelezaji wake katika Robo ya Tatu ya mwaka wa fedha.
Katika Ziara hiyo wameweza kukagua miradi Mbalimbali katika Manispaa hiyo ikiwa ni Ujenzi wa Barabara ya Olympio yenye kilometer 0.680 (DMDP) kwa kiwango cha lami, ujenzi wa Barabara ya Mbaruku Km.0.380 iliyopo kata ya Upanga Mashariki ambapo mradi hiyo ilianza Januari 23 ,2017 hadi Januari 22, mwaka 2018 na miradi hiyo imekamilika .
Miradi mingine ni Ujenzi wa Madarasa 4 ya Gorofa Shule ya Sekondari Gerezani, na Ujenzi unaendelea, Ukarabati wa vyumba vya Madarasa 27,Kumbi 2 pamoja na Jengo la Utawala Katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko ambapo mradi huo umekamilika.
Katika Ujenzi wa Ofisi za Afisa Mtendaji kata katika kata za Bonyokwa na Liwiti Ujenzi unaendelea
Imeelezwa kuwa kuna baadhi ya changamoto zianzokumba miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kutowekwa taa katika Barabara ya Olympio pamoja na Miradi kuchelewa kukamilika kulingana na Muda uliopangwa.
Tazama Picha zikionyesha miradi mbalimbali ambayo yametembelewa leo na kukagua utekelezaji wake katika Halmashauri ya Ilala.
Ofisi ya Afisa Mtendaji kata Liwiti.
Ofisi ya kata Bonyokwa
Ujenzi wa Tenki la Maji lenye Ujazo wa Lita 150,000 Kisukuru.
Barabara ya Segerea Bonyokwa yenye Km.2.0 kwa kiwango cha lami.
Wakikagua shimo lililopo Barabara ya Olympio Upanga Mashariki lililowekwa kwa lengo la kuwekwa nguzo ya Taa.
Shimo kwa ajili ya Kuwekwa nguzo ya Taa katika Barabara ya Olympio.
No comments:
Post a Comment