Wamiliki wa vyombo vya usambazaji habari
kama vile blogu, TV na redio za mitandaoni nchini Tanzania wametakiwa
kujisajili na kufuata maadili kwa mujibu wa kanuni husika.
Hatua hiyo inajiri baada ya serikali kushinda kesi iliofunguliwa na wadau wa habari kupinga kanuni za maudhui mitandaoni 2018.
Kulingana na taarifa hiyo iliochapishwa
na mkurugenzi wa idara ya habari na maelezo na msemaji mkuu wa serikali
Daktari Hassan Abbasi, walalamishi waliwasilisha maombi ya kupata ridhaa
ya kufungua shauri la kufanyiwa marejeo kanuni hizo zilizosainiwa na
waziri mwenye dhamana ya habari ambazo pamoja na mambo mengine
zinasimamia zinasimamia usajili na kuweka mfumo wa uwajibikaji na
maadili kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii inayohusika na habari.
Katika
kesi hiyo, serikali iliweka pingamizi tatu za kisheria ambapo pamoja na
mambo mengine iliomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa
walalamishi hawakuthibitisha kuwa wana haki ya kikatiba ambazo
zitavunjwa na kanuni hizo, hoja ambazo zilikubaliwa na mahakama
kuyatupilia mbali maombi hayo.
''Kwa hukumu hiyo , tunatumia fursa hii
kuutarifu umma kuwa sasa wamiliki wa mitandao ya kijamii inayohusika na
usambazaji wa habari kama blogu, TV na redio za mitandaoni na wengine
walioainishwa katika kanuni wanapaswa kuendelea kujisajili na kufuata
maadili kwa mujibu wa kanuni husika'', ilisema serikali katika taarifa
hiyo.
Serikai ilisema kuwa wale wanaotuma
maombi watahitajika kuwasilisha stakhabdhi zao ikiwemo maelezo ya hisa,
uraia, kibali cha kuonesha wanalipa kodi mbali na mipango ya mafunzo.
Wanablogu ambao wataopatikana na hatia
ya kutoheshimu sheria hizo mpya watakabiliwa na faini ya hadi milioni 5
ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama zote mbili kulingana na sheria
hizo mpya, ilisema taarifa hiyo.
Rais Magufuli alitoa agizo la
kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayechapisha habari za
uongozi kuhusu serikali katika mitandao ya kijamii.
Idadi ya watumiaji wa mitandao nchini Tanzania ilipanda hadi asilimia 16, 2017.
No comments:
Post a Comment