Na Heri Shaaban
SERIKALI ya Mtaa ya Upanga Mashariki imesema vitendo vya uhalifu katika mtaa wao kwa sasa vimepungua baada kuanzishwa Ulinzi Shirikishi wa madereva wa bodadoda wa mtaa huo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana, na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Rukiya Ritani, wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya mtaa wake.
"Tumeanzisha Polisi jamii katika mtaa wetu jeshi letu la madereva wa bodaboda wanafanya kazi zao kwa umakini kwa sasa vitendo vya uhalifu amna tukio la uhalifu likitokea wanawakamata watuhumiwa alafu wanapelekwa polisi"alisema Rukiya .
Rukiya alisema wananchi wake wa mtaa huo kwa ushirikiano wa Wajumbe wake wa serikali ya mtaa wanashirikiana na Polisi Jamii katika kulinda rahia na mali zao.
Alisema kwa sasa mafanikio makubwa ambayo yamepatikana wananchi wanapita bila kupolwa barabarani mali zao.
Alisema mtaa huo una wakazi 4800 changamoto iliyokuwepo walipaji ada wachache amewataka wananchi kulipa ada ya ulinzi kwa wakati ili iweze kuwasaidia polisi jamii wao ambao wanafanya kazi hiyo ya kujitolea.
Akielezea changamoto nyingine wanachi wa mtaa huo wamekuwa wavivu katika kushiriki vikao vya maendeleo jambo linapotokea katika mtaa mengi wanaoitwa.
Kwa upande wake kiongozi wa Ulinzi shirikishi Upanga Mashariki, Seleman Abdalah alisema asilimia 85 uhalifu umepungua.
Abdallah alisema kwa sasa Upanga Mashariki mpya jeshi lake limejipanga vizuri wanashirikiana na Polisi wakati wa matukio ya uhalifu yakitokea.
No comments:
Post a Comment