A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, May 13, 2018

Tshishimbi arudi kwao haraka





AKIJIUGUZA kwa muda wa wiki mbili bila matarajio ya kupona, kiungo mkabaji wa Yanga Mkongoman, Papy Kabamba Tshishimbi ameamua kurudi kwao fasta kwa ajili ya kwenda kujitibia kwa miti shamba.

Kiungo huyo yupo nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili akiuguza majeraha yake ya enka aliyoyapata katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika walipokutana na Wollayta Dicha ya Ethiopia na hata kwenye mchezo dhidi ya Rayon Jumatano, hatakuwepo.

Staa huyo aliyewabamba mashabiki wa Yanga, hadi sasa amekosa mechi mbili dhidi ya USM Algier’s na ile ya Prisons na hata ya leo Jumapili na Mtibwa mjini Morogoro ataikosa.

Habari za ndani zinasema kwamba amerudi kwao baada ya kutoridhishwa na matibabu aliyokuwa akipata hapa nchini na amewaambia viongozi kuwa kuna sehemu kule kwao anaweza kupata dawa za kienyeji zikamrudisha kwenye hali nzuri.

Kocha wa Yanga, Zahera Mwinyi alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo alisema; “Ni kweli Tshishimbi hayupo na timu ana majeraha ya enka aliyoyapata katika mechi za nyuma. Yeye hayupo katika timu kwa muda wa siku nne akiendelea na matibabu.”

KUIVAA MTIBWA
Yanga inaivaa Mtibwa leo Jumapili mjini Morogoro kuwania Sh41milioni ambazo ni zawadi ya mshindi wa pili wa Ligi Kuu Bara lakini ni kama robo ya mshahara wa wachezaji wake kwa mwezi mmoja. Kikosi hicho kilichovuliwa ubingwa na Simba, hakijashinda mechi hata moja tangu kikimbiwe na Kocha wake Mkuu, George Lwandamina na takwimu zinaonyesha kwamba kila mwezi kinatumia Sh115milioni kulipa mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi.

KAKOLANYA AUMIA
Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya aliumia kwenye mazoezi ya timu hiyo ya jana na kurejeshwa Dar es Salaam, nafasi yake akaitwa Youthe Rostand aliyekuwa amebaki Dar es Salaam akijiandaa na kikosi kitakachoivaa Rayon

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages