A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 1, 2018

Taasisi ya Haftrade inajenga madarasa mawili Handeni




Na Heri Shaaban,Handeni Tanga

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Haftrade Iliyopo Handeni Mjini Mkoani inajenga madarasa mawili katika wilaya hiyo ili kuungana na serikali katika mpango wa elimu bure.

Akizungumza katika ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa mwishoni mwa wiki Handeni Mjini Mkoni Tanga Mkurugenzi wa Taasisi ya Haftrade Thecla Mingwa alisema ujenzi wa madarasa hayo yapo katika hatua za mwisho ili kuwezesha wanafunzi kusoma.

Mingwa alisema Hafrade ina wanachama hai 20 mpaka sasa, ni taasisi iliyosajiliwa inashughulika na shughuli za kijamii ikiwemo, elimu,Mazingira,Afya na Maji vijijini.

"  Taasisi yangu ya Hafrade  wakati ikiendelea kusimamia ujenzi huo mkakati wake kutafuta wadau kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari ya Kwenjugo, pia kutoa elimu pamoja na kupanda miti ya matunda na mikorosho" alisema Mingwa.

Mingwa alisema shirika lao mikakati mingine liwe pana Kimkoa hadi Taifa wawe wabunifu katika kusimamia kazi za Serikali ya awamu ya tano .

Aidha alisema mikakati mingine kuwa na mashamba makubwa kuyaendesha kwa kilimo .

Alisema Hafrade inashirikiana na Shirika la Save Childern  katika shughuli zake mbalimbali katika kuleta maendeleo.

"Hafrade inatoa huduma zake Handeni Mjini yenye Kata, 12 ambazo ni Chanika, Kidereko, Konje, Kwamagome,Kwediyamba,Kwenjugo Mangaribi   ,Kwenjugo Mashariki,Mabanda,malezi ,mlimani, msasa na vibaoni"alisema.

Mingwa alisema katika utendaji wa shughuli zake Haftrade imegawanyika katika idara nne ambazo ni idara ya elimu, idara ya Afya, idara ya mazingira, na idara ya maji na inaendesha shughuli zake kwa kushirikiana na serikali kuakikiasha malengo na mikakati iliyopangwa inatumia.

Alitaja kazi za baadhi ya idara hizo kuwa ni Idara maji kulinda vyanzo vya maji, idara ya mazingira kuandaa maeneo ya shamba kwa ajili ya kilimo cha shamba darasa.cha mihogo na korosho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages