Tuzo hiyo aliyopewa Shilole ilitolewa siku ya Mama duniani ambapo ndiyo siku ambayo Aunty Ezekiel alizindua short Film yake ya Mama ikiwa ni ujumbe kuhusu kwa wa mama wote Duniani na namna wanavyopambana kulea watoto wao katika mazingira magumu.
Wakati wa ukabidhiwaji wa Tuzo hiyo Shilole hakuwepo hivyo Snura akamuwakilisha na ndipo leo kupitia Instagram page ya Shilole ameamua kuandika haya...”Naamini wapo wengi mno waliostahiri, lakini siwezi kuwa na maneno ya kutosha kukushukuru kwa heshima kubwa uliyonipa Mama Cookie.”
“Asante kwa zawadi nzuri, heshima na Tuzo ya mama mpambanaji bora kwa bongo flavour na movie, ktk uzinduzi wako wa filamu ya Mama. Lkn pia hongera kwa kazi nzur na product ya body spray uliyoizindua wewe ni Mwanamke Shupavu.”
“Mama yangu Aliniacha nikiwa mdogo sn nikaelewa ilivyo vigumu kuishi bila Mama. Ndio maana Pamoja na yooote Nitapambana kwaajili ya wanangu. Ukiwagusa wanangu, Umenigusa mimi. Ndio watu pekee naoweza kusema Nipo tayar kufa kwaajili yao.” – Shilole
No comments:
Post a Comment