A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 31, 2018

Sera mpya ya Maendeleo ya Vijana itawawezesha vijana kuinuka kiuchumi



Na Heri Shaaban.

IMEELEZWA kuwa sera ya Maendeleo ya Vijana itawezesha kundi kubwa la vijana kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa malengo ya Dunia (SDG's) ifikapo mwaka 2030.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam Jana,na Peter Kalonga Mwakirishi wa KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu katika ufunguzi wa mkutano wa vijana wa Mkoa Dar es Salaam,Pwani,na Morogoro wakati wa kujadili ukusanyaji maoni ya rasimu ya Sera mpya ya Maendeleo ya VIJANA.

Kalonga alisema malengo ya kimkakati yatawezesha vijana kutumia vizuri fursa za Maendeleo zitokanazo na ukuaji wa sayansi na teknorojia.

"Sera hii ya Maendeleo ya vijana  ambayo inajadiliwa itasaidia makundi ya VIJANA kushiriki kikamilifu katika utekekezaji wa malengo endelevu katika upatikanaji wa sera Mpya vijana"alisema Kalonga.

Kalonga alisema Ofisi ya Waziri MKUU imeamua kufanya mapitio ya sera ya Maendeleo ya vijana kwa sababu ,Serikali inatambua kuwa vijana ni rasilimali watu muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya kiuchumi na kijamii Katika Taifa let.

Alisema takwimu Za Maendeleo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa asilimia 35 ya Watanzania wote ni vijana wenye umri 15,Hadi 35 na asilimia 56 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana wenye umri huo huo.

Aidha alisema sababu ya kupitia Sera iliyopo ni kwamba ina mambo mengi ya kijamii,kisiasa yanajitokeza ambayo yatapelekea kuwepo haja ya kufanya mabadiliko katika sekta

Kwa upande wake Ofisa VIJANA Mkoa Dar E Salaam Masalida zephania alisema serikali inafanya kila jitihada kuwahudumia vijana na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli zenye tija kwa ajili ya Maendeleo ya TAIFA.

Zephania alisema aliwataka vijana wajadili kwa kina na kutoa mawazo yao katika masuala mbalimbali  ikiwa pamoja na tafsiri ya kijana wa Tanzania, uzalendo na Utaifa,afya,ajira ,elimu, umuhimu wa teknolojia ya Habari na mawasiliano na ushirikishwaji wa VIJANA katika mchakato wa Maendeleo.

Alisema Tanzania in vijana milioni 6 na mwaka jana serikali ilitenga bilioni 12.5 kwa vijana wote nchini na pesa hizo zilisambazwa kila Halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri mkuu
James Kalugusi alisema mafunzo hayo yameshirikisha vijana 150 wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

James alisema sera ya Taifa ya miaka mitano inaangalia mikakati ya kusaidia vijana kuanzia miaka15 na sera ya afya Taifa uzazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages