A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 19, 2018

Sanlam na Maxcom kuwawezesha wateja wa bima kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi

01%2B%25281%2529
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa pili kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakisaini  hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
02
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa tatu kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
03
Baadhi ya maofisa wa Maxcom  wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wa Sanlam Life Insurance katika hafla hiyo.
04
Baadhi ya maofisa wa Sanlam Life Insurance  wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wa Maxcom katika hafla hiyo.

WATANZANIA watapata fursa ya kufanya malipo ya bima mbalimbali kwa njia rahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi baada ya kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Maxcom kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara.

Akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman alisema kwamba sheria ya bima imebadilika hivyo kuwataka wateja wa bima kuweza kufanya malipo yao  moja kwa moja kwenye kampuni za bima.

“Sheria ya bima huwa zinabadilika mara kwa mara kwa sasa sheria inamtaka mteja wa bima kuweza kufanya malipo bila kupitia kwa dalali au mawakala wa bima na tumegundua njia rahisi ya kuwawezesha wateja wetu ni hii ya kuweza kufanya malipo ni kupitia simu zao za mikononi,” aliongeza Suleiman.

Aliongeza kwamba utaratibu huo wa kulipa malipo ya bima kwa njia ya simu za mikononi unalenga kupanua wigo wa kulipa malipo na kuimarisha makusanyo ya michango na kumsaidia mteja wao kufanya malipo kwa njia rahisi zaidi ndani na nje ya nchini.

Aliongeza kwamba kwa takwimu za hivi karibuni takribani asilimia 62 ya watanzania wana miliki simu za mikononi ambapo ni sawa na watu milioni 20 lakini wanaofanya malipo ya bima  hawazidi laki moja.

“kwahiyo tumeamua kuungana na hawa ndugu zetu wa Maxcom ili kuweza kuwarahisishia wateja wetu kuweza kufanya malipo ya bima kwa njia ya simu za mkononi” aliongeza Suleiman

Kwahiyo alisisitiza umuhimu wa kuingia kwenye malipo kwa njia ya simu kwa kuwa kwa mwaka watanzania wanaofanya malipo kwa njia ya simu za mkononi ni wengi na takribani shs bilioni 1.4 kwa mwaka miamala kwa njia ya simu hufanyika.

Suleiman alisema ni muhimu kuweza kuingia kwenye soko hilo ili kuweza kuongeza wigo wa soko lake ambalo kwa sasa alisema kampuni hiyo ina asilimia 62 kwenye soko la bima nchini na kwa mwaka jana pekee kampuni yao ililipa madai kwa wateja wake kiasi cha shs billion 14.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson Kasati alifafanua kwamba mfumo wa kampuni yao wa kielectroniki ni imara na salama kwa wateja wa bima nchini kuweza kufanya malipo mbalimbali kama michango na kulipa ada kwa wakati wakiwa mahali popote.

“tumejiunga na ulipaji wa njia ya kieletroniki na serikali ambapo pia watu na makampuni binafsi wanaweza kupata fursa hiyo ya kufanya malipo yao kwa njia ya simu za mkononi katika juhudi za kuboresha ulipaji wa huduma mbalimbali nchini,” alisema Kasati
Aliongeza kwamba uzinduzi wa huduma hiyo ni wakati muafaka wa watanzania kuweza kufanya malipo yao ya bima kwa njia ya simu za mkononi kwa mawakala mbalimbali ndani ya nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages