Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya
Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa pili kushoto), na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakisaini hati za
makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali
kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya
Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa tatu kushoto), na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakibadilishana hati za
makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali
kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
Baadhi ya maofisa wa
Maxcom wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wa Sanlam
Life Insurance katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa
Sanlam Life Insurance wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na
viongozi wa Maxcom katika hafla hiyo.
WATANZANIA watapata fursa ya kufanya malipo ya bima
mbalimbali kwa njia rahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi baada ya kampuni
ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Maxcom kuingia makubaliano ya ushirikiano
wa kibiashara.
Akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi
makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life
Insurance, Khamis Suleiman alisema kwamba sheria ya bima imebadilika hivyo
kuwataka wateja wa bima kuweza kufanya malipo yao moja kwa moja kwenye kampuni za bima.
“Sheria ya bima huwa zinabadilika mara kwa mara kwa
sasa sheria inamtaka mteja wa bima kuweza kufanya malipo bila kupitia kwa
dalali au mawakala wa bima na tumegundua njia rahisi ya kuwawezesha wateja wetu
ni hii ya kuweza kufanya malipo ni kupitia simu zao za mikononi,” aliongeza
Suleiman.
Aliongeza kwamba utaratibu huo wa kulipa malipo ya
bima kwa njia ya simu za mikononi unalenga kupanua wigo wa kulipa malipo na
kuimarisha makusanyo ya michango na kumsaidia mteja wao kufanya malipo kwa njia
rahisi zaidi ndani na nje ya nchini.
Aliongeza kwamba kwa takwimu za hivi karibuni
takribani asilimia 62 ya watanzania wana miliki simu za mikononi ambapo ni sawa
na watu milioni 20 lakini wanaofanya malipo ya bima hawazidi laki moja.
“kwahiyo tumeamua kuungana na hawa ndugu zetu wa
Maxcom ili kuweza kuwarahisishia wateja wetu kuweza kufanya malipo ya bima kwa
njia ya simu za mkononi” aliongeza Suleiman
Kwahiyo alisisitiza umuhimu wa kuingia kwenye malipo
kwa njia ya simu kwa kuwa kwa mwaka watanzania wanaofanya malipo kwa njia ya
simu za mkononi ni wengi na takribani shs bilioni 1.4 kwa mwaka miamala kwa
njia ya simu hufanyika.
Suleiman alisema ni muhimu kuweza kuingia kwenye
soko hilo ili kuweza kuongeza wigo wa soko lake ambalo kwa sasa alisema kampuni
hiyo ina asilimia 62 kwenye soko la bima nchini na kwa mwaka jana pekee kampuni
yao ililipa madai kwa wateja wake kiasi cha shs billion 14.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson
Kasati alifafanua kwamba mfumo wa kampuni yao wa kielectroniki ni imara na
salama kwa wateja wa bima nchini kuweza kufanya malipo mbalimbali kama michango
na kulipa ada kwa wakati wakiwa mahali popote.
“tumejiunga na ulipaji wa njia ya kieletroniki na
serikali ambapo pia watu na makampuni binafsi wanaweza kupata fursa hiyo ya
kufanya malipo yao kwa njia ya simu za mkononi katika juhudi za kuboresha
ulipaji wa huduma mbalimbali nchini,” alisema Kasati
Aliongeza kwamba uzinduzi wa huduma hiyo ni wakati muafaka
wa watanzania kuweza kufanya malipo yao ya bima kwa njia ya simu za mkononi kwa
mawakala mbalimbali ndani ya nchini.
No comments:
Post a Comment