A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 22, 2018

RITTA KABATI CHALLENGE CUP MSIMU 2018 WAFUNGULIWA RASMI,TIMU ZAOMBWA KUCHUA FOMU KUSHIRIKI


kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo  vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani Iringa mapema hii leo

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Kamati ya ya mshindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha radio cha Nuru Fm.

“Naomba viongozi wa vilabu vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya nambari 0714201006  au mnipigie mimi mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela

Malekela alisema kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani Iringa,Kuonesha uwezo wa vijana na kutengeneza ajira  kwao,Kujenga kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi,Kutoa burudani kwa wakazi wa iringa kwa  mchezo wa mpira wa miguu,Kuwakutanisha vijana pamoja ili kuzungumza lugha moja ya kimichezo na maendeleo,Kuwaepusha vijana na makundi au vijiwe visivyo faa na Kuhamasisha michezo katika mkoa wa Iringa,kutimiza agizo la makamu wa raisi juu ya kufanya mazoezi

“Sasa hapo utagundua kuwa jinsi gani mashindano hayo yalivyo yanaumuhimu katika kukuza vipaji hapa mkoani kwa ustawi wa soka letu la nchi hiii” alisema Malekela

Aidha Malekela  alizitaja zawadi pamoja na vifaaa ambavyo vitatolewa kwa timu shiriki


VIFAA
 msimu wa mwaka huu wa 2018 Kupitia mdhamini RITTA KABATI tunataraji kutoa vifaa  vya michezo kama ifuatavyo kwa timu shiriki.
Kifaa
Muhusika
idadi
Mipira ya mazoezi
Timu shiriki
Mpira mmoja (1)
Jezi za mechi
Timu shiriki
Jezi set 1
Jezi za waamuzi
Waamuzi
Set 6

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages