A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, May 20, 2018

RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO

*RC MAKONDA AZINDUA KAMATI YA KUPITIA SHERIA YA NDOA NA MIKATABA YA KIMATAIFA INAYOHUSU HAKI YA MTOTO*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amezindua Kamati ya Watu 18 kutoka makundi mbalimbali aliyoiunda kufanya Mapitio kasoro zilizoonekana kwenye Sheria ya Ndoa wakati wa zoezi la kutafuta haki ya Mtoto kisha kutoa mapendekezo kwa lengo la kuweka Ustawi bora wa Mtoto.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Albert Msando ambae ni wakili wa kujitegemea, Katibu Florah Masue pamoja na wajumbe 16 wakiwemo Wanasheria, Maafisa ustawi wa jamii, Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na wajumbe kutoka taasisi za kutetea haki ya mtoto ambao watakaofanya uchambuzi wa kina wa kisheria kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo.

RC Makonda amesema baada ya kukamilika kwa ripoti ataikabidhi kwa Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Afya pamoja na Wizara ya Katiba na sheria kwaajili ya kuwasilishwa Bungeni
Aidha RC Makonda amesema miongoni mwa vitu vitakavyoshughulikiwa ni pamoja na mapitio ya Sheria ya mtoto ya mwaka 2009, Muundo wa Mahakama za watoto, kiwango cha fedha ya matunzo ya mtoto kama kinakidhi hali ya sasa, Mamlaka ya Ustawi wa jamii pamoja na kuangalia sheria za kimataifa.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema Zoezi la kutafuta haki ya mtoto limekuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya watu 7,000 walisikilizwa, familia 2008 wameanza kupatiwa pesa ya matunzo, 2,971 watapatiwa kadi za bima ya afya, 90 wamepimwa DNA huku wananchi 10,000 wakishindwa kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages