Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.
Pendekezo la John Bolton liliighadhabisha na kuitia wasiwasi Korea Kaskazini ambayo ilitisha kujitoa kwa mkutano na Trump wa mwezi ujao.
Mwaka 2003 kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ili apate kuondolewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.
Hata hivyo aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi miaka kadhaa baadaye, mfano ambao ulionekana kumtia wasi wasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Pyongyang ilionya Jumatano kuwa huenda isihudhurie mazungumzo hayo ambayo yanapangwa kufanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni.
No comments:
Post a Comment