A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 2, 2018

Rais Magufuli atoa ahadi hii kwa Wafanyakazi Baada ya Kushindwa Kuwapandishia Mishahara Mwaka Huu

Katika hotuba yake  kwenye maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa, Rais Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa kiasi kikubwa kabla hajamaliza awamu yake ya uongozi.

''Kipindi changu cha Urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'', amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameweka wazi kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza kabla ya kupandisha.

"Natamani mwaka huu kupandisha mishahara kwa wafanyakazi lakini kutokana na changamoto zilizopo za kuajiri wafanyakazi 52,000 nitawalipa nini? nikisema natamka kuongeza mishahara, nitazipata wapi?”amesema Magufuli.

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.

Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA)  Tumaini Nyamhokya, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages