A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 10, 2018

Rais Magufuli anashahili kupongezwa - Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaama Paul Makonda amepongeza jitihada za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba zinastahili pongezi na haoni ni sababu zozote za baadhi ya watu wanaompinga.

 Amesema hayo leo Mei 10, 2018, wakati wa kupokea ripoti ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa soko la Mbagala, kituo cha kisasa cha daladala Chamazi na kile cha Tuangoma na kusema kuwa kwa watu ambao wanapinga jitihada hizo wana matatizo ya akili au wapo upande wa shetani.

“Niendelee kuwasihi wananchi, yeyote yule atakaye waambia hakuna chochote kinachofanyika na kutendeka ujue kwamba ni tatizo la akili au ameuamua kukaa upande wa shetani kwa kupinga hata mambo mema yanayofanywa na Rais Magufuli, unampinga kwa kujenga stendi ya Ubungo ya kukupatia zaidi ya bilioni 50? unampinga kwa kujenga Standard Gauge? unampinga kwa kuleta Bombardier? Au unampinga kwa kupanua bandari?",  amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa serikali kuu kupitia Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Fedha na Mipango imetenga kiasi cha shilingi bilioni 250 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.

Mkuu mkoa pia alielezea baadhi ya miradi mbalimbali ambayo serikali imetekeleza na ile ambayo ipo mbioni kukamilika katika mkoa wa Dar es salaam ikiwemo, upanuzi wa bandari ya Dar es salaam, miradi ya ujenzi wa barabara, kituo cha mabasi Mbezi, Soko la Kisutu, Mradi wa mabasi ya mwendokasi awamu ya pili.

Makonda aliwasihi wakurugenzi waliopo katika jiji la Dar es salaam ambao ni wasimamizi wakuu wa fedha, kutokuwa na uwoga wa kuchukua hatua kwa mtu yeyote kwasababu wao ni wateule wa Rais John Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages