A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 17, 2018

POLISI WAIBUA BALAA ISHU YA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA!


DAR ES SALAAM: Huu mchezo wa baadhi ya wanaume kuona wanawake wenye makalio makubwa na kujifanya kurukwa na akili kwa kuwapigia miruzi, kujikohoza au kuzomeazomea umefikia mwisho.
Jeshi la polisi na hasa Visiwani Zanzibar liko ‘siriazi’ na ishu hii ambapo hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Magharibi ‘RPC’, Hassan Nassir (pichani), alitoa tamko ambalo limeibua balaa mitaani.

SIKIA TAMKO LA RPC
Hebu kabla ya kuelezea balaa lilolopo kuhusu tamko hilo ni bora kujipa muda wa kumsikiliza RPC Nassir kile alichosema alipozungumza katika semina ya kulinda utu wa mwanamke na mtoto iliyofanyika hivi karibuni mkoani humo.
“Naomba wananchi wajue mwanamke kupita pengine maumbile yake yamejazajaza ukaanza kukohoa, mmh, mmmh, hilo ni shambulio la aibu tutakukamata tukupeleke mahakamani.
“Maana wengine wanafikiri ni mchezo tu ina maana mama zetu, dada zetu, watoto wetu wenye maumbile makubwa wasitembee mitaani; maana wakitembea watu wanaanza kukohoa mmh, kama una kihozi nenda kwako ukakohoe ndani huwezi kuwa mwanamke kupita hapo unaanza kukohoa hilo ni shambulio la aibu.

BALAA LILILOPO
Siku chache baada ya kutolewa kwa tamko hilo la RPC Nassir mitandao ya kijamii ilishiba hoja hiyo huku mawazo ya wengi yakitofautiana.
Wapo waliosema kwamba amri ya kuwakamata wanaowadhalilisha wanawake kwa kuwapigia miruzi itaishia Visiwani Zanzibar kwa sababu aliyeitoa si mkuu wa Jeshi la Polisi.
Mbali na agizo hilo kuleta mkanganyiko huo wa sura ya kitaifa baadhi ya wanaume walionekana kutishika na hali ya kutaniana kati ya mtu na mtu nayo haikubaki nyuma.

AMANI LAMTAFUTA RPC
Pamoja na uwepo wa video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha RPC Nassir akitoa tamko hilo, Amani lilimtafuta mkuu huyo wa polisi mkoa ili kuomba ufafanuzi zaidi.
Amani: Tumeona kuna video inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikikuonesha ukikaripia vitendo vya baadhi ya wanaume kuwadhalilisha wanawake; tungependa kujua kama ni yako na nini msingi wake.

RPC Nassir: Ndiyo hiyo ni yangu, nimeitoa jana (Jumatatu, Mei 14 mwaka huu) msingi wangu ni kulinda utu wa mwanamke, haifai kuwafanya wenye makalio makubwa wajione kama vioja mitaani, waone aibu kutoka majumbani kwao kwa kuhofia watazomewa au kuchekwa, haiwezekani.
Amani: Wewe ni kamanda wa mkoa, watu wanasema huwakilishi jeshi lote la polisi, hii marufuku yako inahusu Zanzibar au na Tanzania Bara kwa ujumla?
RPC Nassir: Naweza nisijibu hili kwa ufasaha kwa sababu sijui sana sheria, lakini katika hali ya kawaida makosa ndani ya nchi yetu na sheria zake zinafanya kazi nchi nzima, huwezi kusema tutawalinda wananawake wa Zanzibar wasifanyiwe mashambulio ya aibu halafu tukaacha wanawake wa Tanzania Bara wakinyanyaswa.
Amani: Umesema utawakamata wote na kuwafikisha mahakamani, ninyi ni polisi mmepanga kuingia mitaani kusikiliza wanawake waopigiwa miruzi ndipo muwakamate watuhumiwa, au mtafanyaje?
RPC Nassir: Tutafanyia kazi malalamiko, ndiyo maana nawaomba wanawake wote nchi nzima wanaofanyiwa vitendo hivyo waripoti kwenye vituo vya polisi ili hatua zichukuliwe, lengo ni kujenga jamii inayoheshimiana, tusilifanyie mchezo jambo hili.

WENGI KUISHIA MAGEREZA
Uchunguzi unaonesha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wanaume na hasa vijana kuwapigia miruzi wanawake wenye makalio makubwa kama ishara ya kupagawishwa na maumbile yao.
Endapo hatua ya Polisi kulivalia njuga jambo hili itakuwa na meno kuna uwezekano wanaume wengi kuingia gerezani kutokana na kupenda kushabikia vitendo hivyo vibaya dhidi ya wanawake wenye makalio makubwa maarufu kama ‘wamejaaliwa.’

WALIOJAALIWA WANASEMAJE
Miongoni mwa wanawake waliojaaliwa waliozungumza na Amani wameonesha kuipongeza hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kwa madai kuwa itawasaidia kulinda heshima yao.
“Ile video niliiona nikadhani ni mambo ya mitandao, lakini kwa kuwa mmesema ni ya kweli nampongeza huyo polisi, wakati mwingine huwa najuta hata kuumbwa hivi, sina raha kila ninapopita mitaani nazomewa utafikiri nimebeba kinyesi,” alisema Joan James binti aliyejaliwa mkazi wa Sinza, Dar alipozungumza na Amani.
RPC Nassir.
MWANASAIKOLOJIA HUYU HAPA
Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya wanaume wengi kuvutiwa na wanawake wenye makalio makubwa jambo ambalo wanasaikolojia wamekuwa wakilielezea kama ni la kisaikolojia zaidi.
“Hisia huleta hamasa haraka, wanaume wengi wanapowatazama wanawake wenye makalio makubwa huwa wanaamini kuwa wana kitu cha ziada kwenye mapenzi na mambo kama hayo, lakini si kweli.
“Ni mhemko tu ambao huwasukuma kuvutiwa nao haraka, lakini uchunguzi unaonesha kwamba wanaume wengi kati ya waliofanya mapenzi na wanawake wa aina hiyo hawakukatwa kiu yao kwa kiwango cha msukumo waliokuwa nao tangu awali,” alisema Chris Mauki mwanasaikolojia maarufu nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages