Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama pamoja na mke wake Michelle Obama wamepata dili nono la miaka mingi katika kampuni ya burudani ya “Netflix” ikiwa ni pamoja na kutimiza ndoto zao kupitia dili hilo.
Kupitia kampuni hiyo ya Netflix Barrack Obama pamoja na mke wake watakuwa ni Production Managers ambao watajihusisha na utengenezaji wa scripts za tamthiliya, makala na filamu.
>>>Kitu kimoja wapo katika maisha yetu ya huduma za jamaii ilikuwa ni kukutana na watu tofautitofauti na kuwasaidia kusambaza uzoefu walionao na watu wengine “ alisema Obama katika maelezo yaliyotolewa na Netflix
“Tutafurahi pia kuinua vipaji na kukuza sauti kwa wale wanaotaka kuelewa na kusambaza hisia pamoja na stori zao kwa jamii na dunia nzima“
Netflix ni kampuni ya burudani iliyopo Marekani iliyogunduliwa mwaka 1997 na inahusisha streaming media, video za online na kutoa DVD
No comments:
Post a Comment