A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

MWANAHERI ANASWA NA KIDUME HOTELINI

NANI alisiyejua kama ubuyu ni mtamu jamani! Na ukitaka kuula vizuri, lazima uupatie nafasi ya kutosha kuumung’unya taratibu! Sasa ubuyu wa motomoto unatonya kuwa, mwigizaji mwenye mvuto Bongo Muvi, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ amenaswa na kidume mwenye asili ya nchini Kongo katika Hoteli ya DS iliyopo Chang’ombe jijini Dar.


MSAMBAZA UBUYU
Msambazaji ubuyu wetu alitonya kuwa, Mwana amekuwa akionekana mara kwa mara kwenye hoteli hiyo, jambo ambalo liliwashangaza wengi kwa sababu wanajua amefunga ndoa hivi karibuni na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Hamis.
“Yaani Mwanaheri anaonekana hapo hotelini mara kwa mara akiwa na huyo mwanaume ambaye siyo yule mume wake.
“Inashangaza maana ndiyo kwanza kaolewa hivi karibuni tu,” alisema mtoa ubuyu huyo.

ANAJIFICHA
Aliendelea kumwaga data kuwa, mara nyingi Mwana akifika katika hoteli hiyo huwa anajificha na kumgundua ni ngumu, lakini kwa vile kuna watu wameshamkariri, ndiyo wanajua kuwa ni yeye.

Ijumaa Wikienda kama kawaida yake, baada ya kupata ubuyu huo lilimtafuta Mwana na alipopewa ubuyu wake amung’unye kidogo alianza kufunguka kama ifuatavyo;
Ijumaa Wikienda: Mwana vipi ndoa inaendeleaje?
Mwanaheri: Mungu ni mwema, ninaendelea vizuri kabisa.
Ijumaa Wikienda: Bado uko na mumeo kweli?

Mwanaheri: Jamani! Ndiyo… niko naye, sasa ningeachika mara hii kweli?
Ijumaa Wikienda: Mbona unaonekana na mwanaume wa Kikongo kwenye hoteli moja huko Chang’ombe?
Mwanaheri: Mmh! Siyo kweli, mimi na mume wangu tulikuwa fungate Golden Tulip (hoteli), lakini baadaye ndiyo tukahamia pale DS (Chang’ombe).
Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia waliokuona naye huyo Mkongo ndiye mumeo?

Mwanaheri: Hapana, ni mtu ambaye anafahamiana na mume wangu, kweli alikuwa anakuja pale mara kwa mara.
Ijumaa Wikienda: Hivyo unataka kusema mumeo anajua kukaa kwako DS?
Mwanaheri: Sasa ataachaje kujua wakati tulikuwa wote?

MUME WA MWANAHERI SASA
Baada ya kumsikia Mwana, Ijumaa Wikienda lilimgeukia mume wake, Hamis ambaye alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alifunguka;
Ijumaa Wikienda: Ningependa kufahamu kuwa fungate yako na mkeo Mwanaheri mliifanyia wapi?
Hamis: Mara ya kwanza tulikaa Golden Tulip (Masaki) kwa siku nne kisha tukahamia katika Hoteli ya DS iliyopo Chan’gombe (Dar) ambapo tumekaa kama wiki tatu!

Ijumaa Wikienda: Kuna taarifa kuwa Mwanaheri alikuwa akionekana hotelini hapo na Mkongo, hii ishu ikoje?
Hamis: Siyo kweli, hapo tulikuwa wote na niliamua kumpa muda mwingi wa kupumzika baada ya harusi. Kama ni Mkongo wanayemsema, mimi najuana naye.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages