Zengwe limeanza tena kuelekea Mkutano Mkuu wa dharura katika klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wanachama wameibuka na kuupinga wakieleza kuwa ni batili.
Felix Makua ni mmoja wa wanachama aliyeibuka na kupinga mkutano huo akidai upo kinyume na katiba ya Simba ambayo haihuruhusu mabadiliko ya katiba.
Akiongea kupitia Radio One, Makua ameeleza kuwa katiba ya Simba inayoenda kupitishwa imefanyiwa uchakachuaji kwa kufojiwa huku akisema mkutano huo hautambuliki.
Mbali na kupinga mkutano, Makua amesema pia katiba ya Simba haihuruhusu kufanya mabiliko yoyote ya kikatiba kupitia mkutano wa dharura na badala yake mkutano mkuu pekee ndiyo huwa unahusika.
Mwanachama huyo ameibuka ikiwa ni siku moja pekee imesalia kuelekea mkutano huo utakaolenga mabadiliko ya katiba yenye madhumuni ya kupitisha rasmi mabadiliko ya kisasa ya uendeshwaji wa klabu hiyo.
Hata hivyo malalamiko hayo yanakuwa kama yanakosa nguvu kutokana na serikali kuyapitisha rasmi japo ikitaka mwekezaji achukue asilimia 49 huku 51 ziende kwa wanachama.
No comments:
Post a Comment