A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, May 18, 2018

Mkutano wa Dharura Kuhusu Ebola Kuhitishwa



Shirika la afya duniani WHO linaanda mkutano wa dharura kujadili hatari ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Jopo litaamua leo Ijumaa iwapo kutangaza hali ya dharura ilio na wasiwasi wa kimataifa itakayochangia muitikio mkubwa zaidi katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Inaaminika kuwa watu 44 wameambukizwa katika mlipuko wa sasa na vifo vya watu 23 vinachunguzwa.

Mji huo ulio na takriban watu milioni moja ni eneo kuu la usafiri katika mto wa Congo, hali inayozusha wasiwasi kwamba huedna virusi hivyo vikasambaa zaidi, na kutishia mji mkuu Kinshasa na nchi jirani.

Kenya yachukua hatua baada ya Ebola kuripotiwa DR Congo
Ebola ni ugonjwa unaoambukiza unaosababisha kuvuja damu ndani ya mwili na mara nyingi waathiriwa hufariki.

Unaweza kusambaa kwa haraka kwa kugusa maji maji yanayotoka mwilini mwa muathiriwa, na mara nyingi dalili za kwanza za ugonjwa huo zilizo kama homa ya kawaida siyo rahisi kuzitambua.

WHO awali lilikiri kwamba lilichukuwa muda mrefu kukabiliana na janga la Ebola katika Afrika magharibi kati ya 2014-2016.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages