A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 3, 2018

MBUNGE SOPHIA MWAKAGENDA ATWAA TUZO YA DUNIA


Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya (CHADEMA) ambaye pia ni Mwanaharakati wa siku nyingi wa Wanawake na Watoto amepewa tuzo ya heshima ya "A Woman of the decade in Public life" iliyotolewa katika Mkutano maalumu wa Woman Economic Forum unaofanyika New Delh India ulioanza tarehe 26 April na utamalizika tarehe 01 May 2018 na unaoshirikisha Wanawake zaidi ya 2000 kutoka pande mbalimbali za dunia wakiwemo Viongozi na wale walioonyesha mabadiliko chanya katika jamii.


Katika mkutano huo Mhe. Sophia pia alipata fursa ya kuongea na Wanawake hao kutoka pande zote za dunia na pia amekuwa mwanamke pekee kwa Afrika Mashariki kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo ni ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa wa muda mrefu katika kusaidia wanawake na watoto nchini Tanzania ikiwemo kielimu, kiafya na kiuchumi ikiwemo juhudi zake anazofanya katika kuwawezesha wanawake katika msaada wa kisheria na katika kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwasaidia vifaa vya kufanyia shughuli zao ikiwemo vyerehani na vifaa vingine.

Habari katika Picha na Anna Peter

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages