A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

Marekani kufungua ubalozi mpya leo mjini Jerusalem



Marekani itafunguq ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.

Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner. Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.

Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.

Mr Trump's decision to move the embassy from Tel Aviv has angered Palestinians, who claim East Jerusalem as the capital of a future Palestinian state.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa

Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.

Ni kipi kitafunguliwa na ni nani atahudhuria?
Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatua kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem. Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.

Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 kuanzishwa taifa la Isreal. Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale amboa watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.

Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.

Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.

Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages