A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 29, 2018

Mama Wema ajichanganya

Mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu, Mariamu Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu mahakamani baada ya kushindwa kutoa nyaraka zinazothibitisha binti yake ameshindwa kufika kutokana na kuwepo nchini India kwa ajili ya matibabu.

Tukio hilo limetokea leo , katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema, ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa na yeye kutoa nyaraka za kusafiria badala ya zile za matibabu.

Wakati Wakili wa Serikali, Constantine Kakula akidai mahakamani kwamba kesi ilitakiwa kusikilizwa ushahidi wa upande wa utetezi lakini mshtakiwa wa kwanza, Wema hayupo, mama Wema alidai msanii huyo ni mgonjwa yuko nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na akawasilisha nyaraka alizodai kwamba zinathibitisha kuwa mgonjwa yuko kwenye matibabu.

Hata hivyo nyaraka hizo baada ya kukabidhi nyaraka hizo kwa Wakili wa Serikali, Kakula alizikagua na kudai kwamba ni nyaraka za kusafiria ambapo na kumuomba mama Wema amuonyeshe mahali ilikoeleza kuhusu matibabu.

Hata hivyo Mama huyo alishindwa kuzielezea na kudai kwamba Wakili wa msanii huyo Albert Msando atakwenda kuzielezea.

Kes hiyo imeghairishwa hadi Juni 13, mwaka huu ambapo  mshtakiwa ametakiwa afike mahakamani na uthibitisho wa matibabu na kama hakutakuwa na uthibitisho, mahakama itatoa amri nyingine yoyote inayofaa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages