Mke wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amefunguka na kumshauri msanii Alikiba na mkewe pamoja na Abdukiba na mkewe kuhusu suala la ugonjwa wa UKIMWI na kuwaambia kuwa wame makini kwani ugonjwa huo ni janga na halina tiba.
Mama Salma alisema hayo usiku wa Jumapili ya wiki hii ambapo wasanii wao walifanya sherehe za kuwatambulisha wake zao hivyo Mama Salma wakati akitoa nasaha zake kwa wasanii hao na wake zao aliwataka kuliogopa janga hilo la UKIMWI.
"Dunia ina maradhi, UKIMWI ni janga, UKIMWI ni hatari hauna kinga wala tiba hivyo ogopeni sana mdudu anayeitwa UKIMWI kuwa mwaminifu kwa mke wako na kuwa mwaminifu mume wako wote, mkiwa waaminifu mtayaepuka haya maradhi ambayo hayana kinga wala tiba, nyinyi wasanii kila mtu anawapenda lakini wapendeni sana wake zenu na nyinyi wapendeni sana waume zenu" alisisitiza Mama Salma Kikwete.
No comments:
Post a Comment