Mratibu wa Kampeni cha ujenzi cha choo cha Mtoto wa kike ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala , Tabu Shaibu (katikati) akizungumzia maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo unaotarajia kufanyika Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Lamada. Kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo na Ofisa Elimu Msingi manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas na kushoto ni moja ya wajumbe wa kampeni hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameamua kuanzisha kampeni maalumu ya ujenzi wa Choo cha mtoto wa kike kwa kuanza na shule zote za msingi katika manispaa hiyo.
Hivyo uzinduzi wa kampeni hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 11 mwaka huu ambapo mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuweza kuwaunga mkono watumishi hao katika kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike katika halmashauri hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mratibu wa kampeni hiyo ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu amesema watumishi wanawake wa manispaa hiyo wanatambua na kuthamini jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya tano na wadau wa maendeleo katika kukabiliana na changamoto za mtoto wa kike na kuamua kuanzisha kampeni hiyo kama mchango wao.
Aidha ameeleza sababu za ujenzi wa choo cha mtoto wa kike, na kusema kuwa kila ifikapo Oktoba 11 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike duniani na lengo la maadhimisho hayo ni kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutetea haki za mtoto wa kike.
"Tafiti zimefanyika kuhusu sababu zinazochangia mahudhurio hafifu ya mtoto wa kike darasani hasa wa darasa la saba na takwimu zao zinabainisha wasichana wa darasa la saba hawahudhurii shuleni kati ya siku nne hadi tano kila mwezi.Vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa kwa wasichana wanaoingia hedhi huleta changamoto kubwa kwao.
"Kutokana na changamoto hiyo watumishi wanawake wa Manispaa ya Ilala wameona wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali na kuendelea kuihamasisha jamii na wadau kujenga choo bora cha kisasa kitakachokuwa rafiki kwa mtoto huyu wa kike,"amesema Shaibu.
Amesema mpango huo endevu unatarajia kujenga vyoo 120 katika wilaya ya Ilala ambapo thamani ya choo kimoja ni shilingi milioni 20 .
"Manispaa yangu ipo katika kampeni endelevu ya ujenzi wa choo cha mwanafunzi wa kike katika shule za msingi mpango huu wa choo lengo kuu kumsaidia mwanafunzi aweze kushiriki masomo katika siku nne hadi tano za mwezi"amesema
Amesema tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusiana na sababu mahudhurio hafifu ya mtoto wa kike darasani hususani wa darasa la saba siku tano za kila mwezi kutokana na vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa Kwa wasichana
Amesema kila mwaka watumishi wa manispaa hiyo wameweka utaratibu wa kukutana (Kichen Paty Gala) na kuunga mkono juhudi hizo na kuendelea kuhamasisha jamii na wadau kuweza kujenga choo bora cha kisasa ambacho kitakuwa rafiki kwa mtoto wa kike ambapo kila mtumishi wa kike ameweza kuchangia shilingi, 50,000..
Kwa upande Ofisa Elimu Msingi Elzabeth Thomas amewataka wadau kuunga mkono kampeni hiyo michango yote ielekezwe katika akaunti ya Manispaa ya Ilala Benki ya CRDB akaunti 0150251270500 .
Elizabeti Thomas amesema kauli mbiu ya siku hiyo ni 'Binti makini Mwamvuli wangu Stara"alitolea mfano kuwa binti makini ni yule ambaye anajitambua na kujaa thamani yake kwa kuwa na maadili mazuri na hodari
Amesema uwepo wa choo cha maalum cha mtoto wa kike kitamwezesha kukaa shuleni kwa muda mrefu kushiriki masomo kikamilifu badala ya kubaki nyumbani wakati wa hedhi hali inayoathiri mtiririko wa maudhurio darasani.
"Wanafunzi wa kike wanakabiriwa na changamoto mbalimbali hii moja ya choo kama manispaa tumeimaliza tumeweza pia kujenga choo cha mfano eneo la Chanika ambacho kitazinduliwa "alisema Thomas
Pia ameongeza kuwa mwaka jana Manispaa hiyo wanafunzi watatu walikutwa na ujauzito mara baada kutokea hali changamoto hiyo ameweza kumshirikisha mkuu wa Wilaya Ilala kumaliza changamoto hiyo ya kupata mimba za utotoni.
No comments:
Post a Comment