A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

Magufuli afanya uteuzi mpya

Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo umeanza rasmi leo Mei 13.

Kabla ya uteuzi wa leo Prof Tumbo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (Center for Agriculture Mechanization and Rural Technology - CAMARTEC).

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages