A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 12, 2018

KIFO CHA BILAL MASHAUZI…SIRI MASTAA KUMLILIA YAFICHUKA

Bilal Mashauzi Akiwa na Wema
KWA wafuatiliaji wa masuala ya burudani Bongo, jina la Bilal Mashauzi siyo geni masikioni mwao. Kwa taarifa tu ni kwamba, kijana huyo aliyekuwa muimbaji wa taarabu amefariki dunia juzi baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kifo cha Bilal kimewaliza mastaa wengi wa kike huku sababu kubwa ikitajwa kuwa kijana huyo enzi za uhai wake amekuwa akiwapa michongo mingi ya kipesa hivyo kuweza kuwa na jeuri ya kutesa Bongo.
Akiongea na Risasi Jumamosi Lulu Semagongo ( Aunt Lulu) alisema kuwa Bilal amewaachia pigo kubwa kwani alikuwa na msaada mkubwa kwao hasa mastaa wa kike.
“Kiukweli aliwasaidia wasichana wengi wa mjini, hata sisi baadhi ya mastaa ametusaidia ‘kutuweka’ kwa watu waliokuwa wakitutoa kimaisha, siwezi kumsema kwa mabaya yake maana kila mtu anachagua aishije lakini muhimu tumuombee, nasi tupo nyuma yake,” alisema Aunt Lulu. 

Hata hivyo, pamoja na kauli hiyo ya Aunt Lulu ambaye hakuona shida kuielezea hadharani, mastaa wengine waliohudhuria msibani hawakutaka kuongea chochote kuhusu kifo cha Bilal.


WAMLILIA MTANDAONI
Licha ya kutotaka kuongea na waandishi wetu kuhusu kifo cha Bilal, baadhi yao waliamua kumlilia kwa kuandika kwenye kurasa zao za Instagram.

Hao ni baadhi ya mastaa walioandika kwenye page zao, lakini wengine walioguswa na msiba huo ni pamoja na msanii wa filamu, Lungi Maulanga ambaye aliongea na Risasi kwa uchungu na kudai kuwa haamini kifo cha kijana huyo ambaye amekufa akiwa mdogo.
“Dah! Bilal ameniumiza sana, amekatika kimchezomchezo jamani, sina la kusema Mungu amempenda cha muhimu mimi namuombea tu,” alisema Lungi.  Pumzika kwa amani Bilal! Gazeti Risasi linatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages