A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 31, 2018

Katika kuadhimisha siku ya Mazingira Wanawake Ilala wapanda Miti Shule ya Kasulu


Katika  kuazdhimisha siku ya mazingira Dunani  Wanawake wa Manispaa ya Ilala, leo wameendesha zoezi la kupanda Miti katika  Shule ya Secondary Kasulu iliyopo  katika halmashauri hiyo ambapo wanafunzi wa shule hiyo wameshirikishwa kikamilifu katika zoezi hilo.
Akizungumza katika zoezi hilo Afisa mazingira wa Manispaa ya Ilala Feada Magesa  amesema  wameamua kuwashirikisha wasichana katika upandaji wa miti ili kuwajengea  moyo wa kupenda Mazingira  na kuweza kushiriki katika kutunza mazingira.



‘’Hii siku tumeitenga  sisi wanawake wa  Ilala ili kuweza kupandikiza moyo watoto wa kike wa sekondari na shule za Msingi kupanda miti katika mazingira yao’’ Alisema.

Aidha amesema  baada ya kutembelea shule mbali mbali katika Manispaa ameona shule hiyo ni mpya na haina miti  hivyo kwa  leo wamepanda miti 110 katika maeneo ya shule hiyo  na amewasisitiza wanafunzi  kuitunza miti hiyo  iweze kukua ili kuhifadhi mazingira ya eneo  hilo, na amewashukuru walimu na wanafunzi kuwapokea vizuri  .

‘’ kwakweli wametupokea vizuri kamaulivyo ona wasichana  wamefurahia sana kushiriki zoezi hili nao wamepanda miti naimani wataituza kwa kuimwagilia maji  hadi itakapokua’’.Alisema Magesa .

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo   Christina Kaswaga  ,ameshukuru idara ya Mazingira kwa kuichagua shule hiyo kupanda miti katika  maeneo hayo  kwani shule zikonyigi na kushirikisha wasichana kaika zoezi hilo kumeleta changamoto kuona kuwa nao wanweza kushiriki uhifadhi wa mazingira  , na ameahidi kuendelea kusimamia kuitunza miti hiyo na mazingira ya shule hiyo.

Kwa upande wao wanafunzi wakike walioshirikia zoezi hilo wameshukuru uongozi wa Mazingira Ilala kuwafikia katika shule yao kwani  baadhi yao kutokanana mazingira wanayo toka hawana maeneo ya kupanda miti na hawajawahi hatata kupanda miti hivyo leo imekuwa siku muhimu sana ambapo wamejifunza na kupanda miti .

‘’Naitwa Rehema Shabani  mimi nilikuwa sija wahi kupanda miti hata siku moja  nimependezewa sana na upandaji miti name kwa mara yangu ya kwa nza nimepanda mti, ntahakikisha mti wangu nautuza hadi uwe mti mkuwa  na utakuwa wa ukumbusho’’.Alisema 



Siku ya mazingira Duniana huadhimishwa kila mwaka  ambapo mwaka  huu itaadhimishwa tarehe 5 Juni ,Yenye kaulimbiu ‘’Mkaa ni gharama tutumie Nishati  mbadala’’.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages