Mkurugenzi wa Taasisi ya Abdulah
Aid, Arif Abdurrahimani, akizungumza na waandishi wa habari habari.
Kamati ya ya kutoa misaada ya kibinadamu iliyo undwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa mhe . Paul Makonda kwaajili ya kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko mkoa wa Dar es salaam , imesema imekamilisha zoezi hilo kwa kuwafikia walengwa wote ambao walipata atha hiyo.
Akizungumza na wa waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo Ubaya Chuma amesema waathika wote walikuwa wametambuliwa wamefikiwa na misaada mbambali ya kibinaadamu ikiwemo kupatiwa Magodoro, vyakula mbalimbali kama Maharage , Mchele,Unga wa ngano na wa mahindi Sukari na mafuta ya kupikia na mahitaji mengine mengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Abdulah Aid, Arif Y. Abdurrahimani ameseama katika kuwapatia watu hao misaada Taasisi mbalimbali zimeshiriki ikiwemo, Taasisi ya Miraji Islamic Center ya Zanzibar , Taasisi ya Abdulla AID na Taasisi yake ,amesema wamefurahishwa na huduma hiyo na wameweza kuzifikia kaya 600 kutoka maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akisoma taarifa ya kamati hiyo George Shinga Mtambalike amesema Jumla ya vitu vilivyotolewa na Taasisi hizo ni pamoja na kilo 2400 za mchele,kilo 360 za Sukari, Mafuta ya kupikia Lita 600,kilo 600 za Maharagwe na kilio600 za Unga wa mahindi.
Aidha amesema misaada mingine iliyo tolewa ni pamaoja na Magodoro 490, mito ya kulalia 490 ,Mashuka 490 pamoja na Net za Mbu.
No comments:
Post a Comment