Na Humphrey Shao
Deni la ujenzi wa Mradi wa Machinga Complex linalodaiwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF kwa Jiji la Dar es Salaam limefikia kiasi cha Shilingi Bilioni 47 mpaka sasa tangu mradi huo ujengwe, amebainisha Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita alipokuwa akitoa taarifa ya deni hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Karimmjee.
“ Niwaeleze Waheshimiwa madiwani kuwa deni hili limeongezeka kwa bilioni 15 zaidi mpaka sasa na limefikia Bilioni 47. Hivyo Jiji tumeshafanya utaratibu wa kuunda kamati ya kuweza kushughulikia tatizo hili kwa kumtafuta Waziri mwenye dhamana aweze kutusaidia katika ongezeko hili la riba” amesema Meya Isaya.
Amesema kutokana na deni hilo kuongezeka siku hadi siku wameunda kamati itakayosimamiwa na RAS wa Mkoa wa Dar es Salaam itakayoshughulika na kulipa hili deni kwa kumuona Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo ili riba iweze kukoma.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati wa kikao cha Madiwani wa Jiji kilichofanyika leo katikaukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akiwasilisha ajenda za kikao cha Baraza la Madiwani jiji.
Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam.
Diwani wa Jiji Akichangia mada katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji ya Jiji Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akichangia mada wakati Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam.
Diwani wa Jiji la Dar es Salaam, Amina Yakubu akichangia mada katika Baraza la Madiwani wa Jiji
No comments:
Post a Comment