Msanii wa filamu mwenye tuzo ya msanii bora wa kiume nchini Gabo Zigamba amesema kuwa hakusema atengenezwe kanumba mwingine bali amenukuliwa vibaya.
Gabo amefunguka hayo kupitia eNewz ya EATV ambapo amesema ametafsiriwa tofauti kutokana na kauli yake kwamba tasnia ya filamu nchini inatakiwa kumtengeneza Kanumba mpya.
“Kiswahili ni kimoja lakini tafsiri ni tofauti kulingana na uelewa wa mtu mwenyewe mimi sikumaanisha kuwa atengenezwe Kanumba mpya kama wanavyodai lakini nilikuwa nikimaanisha kuwa uwajibikaji na kufanya kazi kwa bidii ndiyo maisha aliyoishi msanii huyo”, amesema Gabo.
Utata huo uliibuka mara baada ya msanii wa filamu Duma kusema kuwa kauli ya Gabo ni kupingana na mwenyezi Mungu maana ndiye atoaye na kutwaa pia. Mengi zaidi amefunguka Gabo hapo chini,
No comments:
Post a Comment