TANZANIA itahitaji kutengeneza mkakati mpya wa maendeleo na kuachana na falsafa za zamani kama itataka kufikia ustawi na kuwa nchi yenye kipato cha Kati.
Mkakati huo katika; masoko, rasilimali na uwezeshaji unatakiwa kuwezesha sera za maendeleo zilizo endelevu kwa kuangalia zaidi changamoto tofauti za maendeleo na kuzikabili kabla ya kuzitumia kubadili harakati za maendeleo.
Kauli hiyo imo katika mdahalo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kuongozwa wataalamu wa uchumi.
Walisema katika mdahalo huo kwamba mkakati wa zamani kuhusu maendeleo kwa kutegemea kuzalisha bidhaa na kuziuza nje una vikwazo vingi hasa katika uzalishaji kutokana na masuala ya teknolojia na hivyo mkakati utakaokuwa jumuishi, unaoratibu kilimo, madini na huduma unaweza kuwezesha kukua kwa uchumi kama ilivyokuwa katika mkakati wa zamani wa uzalishaji kwa ajili ya kupeleka nje.
Wamesema katika mkakati huo mpya serikali inatakiwa kufanya wajibu mkubwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kimkakati kuelekea uchumi jumuishi ambapo kila mwananchi atashiriki.
Uchumi huo hautategemea uzalishaji wa viwandani pekee bali uchumi wa kisasa unaozingatia huduma ambao katika awamu ijayo kilimo cha kisasa nchini Tanzania kitakuwa sehemu ya mkakati huo.
Wanazuoni hao wamesema kwamba mafanikio ya kuwa na uchumi jumuishi kwa nadharia za sasa zinategemea mpango mkakati wa maendeleo wenye kuangalia mambo mengi yatakayowezesha kuwa na ukuaji jumuishi, unaoshirikisha na kuzingatia uwiano wa masoko, serikali na jamii.
Walisema taratibu hizo mpya duniani zitasaidia kuwa na uchumi wenye mafanikio unaobadili maisha ya watu kwa kuangalia changamoto mbalimbali ikiwamo vifo na kutengeneza mfumo mpya wenye kuzingatia uwezo na mahitaji.
Prof. Basu alizungumzia misingi ya maendeleo kwa kuzingatia sosholojia na saikolojia ya watu. Katika mazungumzo yake aligusia nadharia za misingi ya uchumi kama zilizvyoonwa na akina Nyerere na Nkurumah na wengineo, akiangalia Azimio la Arusha na maendeleo ya binadamu nadharia ambazo zinashabihiana na msimamo wa Stockholm.
Aidha katika mada yake alizungumzia uratibu na udhibiti kama kitu muhimu katika soko na kuona mipango inavyotakiwa kuzingatia watu ambao washiriki katika ujenzi wa uchumi badala ya serikali kufanya makosa ya kudhani watu wanatakiwa kufanyiwa kila kitu,
Prof. Stiglitz yeye alizungumzia kutoka uzalishaji unaolenga soko la nje hadi ukuaji uchumi jumuishi wa karne ya 21 kwa taifa la Tanzania.
Katika majadiliano washiriki walisema kwamba hakuna tishio la roboti kuchukua nafasi za kazi na kuzungumzia haja ya kubadili kilimo ili kuwa msaada mkubwa katika uchumi jumuishi.
Katika majibu ya hoja mbalimbali zilizotolewa na washiriki Prof. Basu alisema kwamba utandawazi si suala la mtu kuudhibiti bali ni namna gani unatumia utandawazi huo kusonga mbele na kusema sera ni muhimu katika maendeleo na kwamba elimu inaweza kusaidia kudhibiti soko.
Naye Prof. Stiglitz alisema kwamba uzalishaji kwa mauzo ya nje hakutasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi kutokana na ukweli kuwa uzalishai huo kwa sasa unakwenda chini na njia mpya lazima kuangaliwa ili kuwa na uchumi jumuishi ulioendelevu.
Mdahalo huo uliwezeshwa na ESRF na kushirikisha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Baada ya mdahalo huo uliokuwa na mafaniko makubwa UDSM, kesho kutakuwa na mkutano wa kitaifa wa 7 mwaka wa ESRF ambao utakaozungumzia Maendeleo ya Binadamu na Uchumi kwa kuzingatia rasilimali zilizopo.
Profesa
wa Uchumi wa Chuo Kikuu Cornel, Ithaca na aliyekuwa mchumi wa Benki ya
Dunia Prof. Kaushik Basu akiwasilisha mada kuhusu misingi ya maendeleo
kwa kuzingatia sosholojia na saikolojia ya watu wakati wa mdahalo kuhusu
uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika
ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Aliyekuwa
mchumi wa zamani wa Benki ya Dunia kutoka Chuo Kikuu cha Columbia,
Prof. Joseph Stiglitz akiwasilisha mada kuhusu kutoka uzalishaji
unaolenga soko la nje hadi ukuaji uchumi jumuishi wa karne ya 21 kwa
taifa la Tanzania wakati wa mdahalo uliowezeshwa na ESRF kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa
Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa mdahalo kutoka kigoda cha Mwl. Julius Nyerere, Prof. Benno Ndulu
akiongoza mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa
Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Mkuu
wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness
Aikaeli akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi
wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akizungumza na kituo cha Habari cha ITV kuhusu mdahalo huo na
manufaa yake kwa Tanzania na kwa sekta ya uchumi wakati wa mdahalo
kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden
uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wakitoa maoni ya mdahalo kuhusu uchumi jumuishi
uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa
Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kutoka
kulia ni Mchumi kiongozi wa Ubalozi wa Sweden nchini, True Schedvin,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF),
Dkt. Tausi Kida pamoja na baadhi ya maafisa kutoka Ubalozi wa Uswidi.
Sehemu
ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na
ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili
wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa
na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya
ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF) mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu
uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika
ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kumalizika kwa
mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden
uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDSM mara baada ya
kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa
Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wahadhiri wa UDSM mara
baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na
ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili
wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment