Lulu Abbas ‘Lulu Diva’
DAR ES SALAAM: Muigizaji wa kitambo kidogo kwenye filamu ambaye hivi sasa ni mtangazaji wa EFM, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amefunguka kuwa lazima atampa kipigo mwanamuziki anayekuja vizuri Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, kwa anachodai hapendi kabisa ajihusishe kimapenzi na kaka yake (mtoto wa mama yake mdogo) ambaye pia ni mwanamuziki, Richard Martin ’Rich Mavoko’.
Akizungumza na Amani, Dokii alisema hajawahi kumpenda mwanamuziki huyo hata kidogo na wala hafikirii kama anaweza kuwa mke bora (Wife Material) kwa kaka yake. “Acha watu waseme mimi mkorofi. Mimi ninayemjua ni wifi yangu ambaye amezaa na Mavoko na si vinginevyo, kiukweli ataniona mimi mtata kwa sababu simuelewi hata kidogo Lulu Diva.
“Safari hii nikimkuta kwa kaka yangu Mavoko siwezi kumuacha lazima achezee kichapo changu kama alivyofanya mama Diamond kwa Mobeto maana kiukweli simpendi kabisa Lulu Diva,” aliapa Dokii. Alipotafutwa Lulu Diva na kusomewa ubuyu huo wa motomoto, alisema yeye hawezi kuumiza kichwa chake kwa kumuwaza na kumuogopa Dokii na kama kinamuuma sana basi aongee na kaka yake.
“Siwezi kumzungumzia Dokii. Kama yeye kinamuuma basi amkataze Mavoko, kwani mimi nina kosa gani? Mwambie aongee na kaka yake,” alisema Lulu Diva.
Alipoulizwa kama anatumia ‘ndumba’ kumtengeneza Mavoko hadi kumsahau msichana aliyezaa naye, alisema si kweli kwani mwanamke anayejiamini hawezi kutumia ushirikina katika kumdhibiti mwanaume.
“Mimi ni mwanamke ninayejiamini na katika maisha yangu yote sijawahi kutumia kabisa hayo mambo (ya kishirikina), sioni umuhimu wake, mtu akinipenda mimi basi ujue kanipenda jinsi nilivyo na mambo yangu,” alitamba Lulu Diva.
Lulu Diva juzikati katika kile kilichoonekana ni kuzuga kuhusu kutoka na Mavoko, alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema: “Mimi na Mavoko hatujawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi, ni mtu wangu, tunasaidiana kwenye kazi.”
No comments:
Post a Comment