Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Sophia Mjema ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Ilala kwa namna walivyojipanga katika kuandaa Maonyesho ya Wajasiliamali aliyoyafunga rasmi tarehe 18 May Mwaka huu.
DC Mjema ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia mamia ya wajasiliamali waliojitokeza kuonyesha na kuuza bidhaa zao katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini DSM,sambamba na kutembelea Mabanda ya Wajasiliamali hao.
Amesema kwa sasa kuna ushindani mkubwa wa Kibiashara na hivyo amewataka Wajasiliamali hao kuhakikisha wanatengeneza bidhaa zenye Viwango vizuri ili kulinda Masoko yao na biashara kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu wa maonyesho hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Almashauri ya Ilala Bi Francisca Makoye amesema kwasasa miongoni mwa wajasiliamali hao wameanza kukua Kibiashara na kuanza kurejesha Mikopo yao iliyowawezesha kufanya biashara.
Katika Hatua nyinge Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema alipata fulsa ya kuwakabidhi tuzo mbalimbali baaadhi ya wajasiliamali wakiwepo Kikundi cha watu wenye Ulemavu wanaofanya shughuli zao ndani ya Jengo la Machinga Complex kwakujihusisha na utengenezaji wa Viatu.
No comments:
Post a Comment