A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 23, 2018

ASHIKILIWA NA POLISI KWA ULAWITI.


Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka

Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa (Nassoro Abdala Nyoya, Sharifa Hassani na Julieta Athanas) kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages