A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 23, 2018

Alikiba na Samatta kuingia dimbani June 9 2018 Uwanja wa Taifa



Mkali wa Bongofleva Alikiba na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wote kwa pamoja wameamua kuwa mabalozi wa elimu wa kujitolea.

Alikiba na Samatta wote wameungana kuhakikisha June 9 2018 watacheza mchezo wa hisani uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia elimu ambapo pesa zitakazopatikana zitaenda kusaidia maendeleo ya elimu nchini.

Kama unajiuliza itakuwaje siku hiyo? basi Samatta ataunda timu yake ya mastaa wa soka na Alikiba pia ataunda timu yake akichagua mastaa wake, mapato ya mlangoni yataenda kuchangia maendeleo ya elimu nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages