BEKI Mtanzania, Abdi Banda, anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Baroka, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili na Mei 2018 kwa upande wa klabu hiyo.
Mchezaji huyo ameisaidia timu yake kufunga mabao mawili na kuiwezesha kwenda sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi uliopigwa Aprili 28 dhidi ya Bloem Celtic katika Uwanja wake wa nyumbani,
Banda amekabidhiwa mpungwa wa rand 5000.00 kama ambavyo klabu hiyo hutoa kiasi cha fedha kwa kila mchezaji bora ndani ya mwezi.
Baroka FC imekshika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 34.
No comments:
Post a Comment