Kufuatia droo ya timu zitakazokutana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kufanyika jana, uongozi Yanga wafurahia kupangwa na timu za ukanda wa Afrika Mashariki.
Ukiachana na USM Alger inayotokea Algeria, Yanga imepangwa na timu za Rayon Sports kutoka Rwanda pamoja na Gor Mahia FC ya Kenya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano kutoka klabu hiyo, Hussein Nyika, ameeleza kuwa wameipokea vizuri droo hiyo kwakuwa inahusisha timu zinazotoka ukanda wa Mashariki.
Vilevile amesema kuwa wanazifahamu vizuri hivyo watapambana kuhakikisha wanazidi kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment